SERIKALI KUFANYA MABORESHO MAKUBWA YA MFUMO WA UNUNUZI

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande, amesema kuwa Serikali imeweka udhibiti wa mianya ya rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma uliosababishwa na kasoro katika Mfumo wa Ununuzi wa Umma (TANePS) kwa kufanya maboresho makubwa ya mfumo huo. Hayo yamebainishwa mkoani Iringa wakati alipofanya ziara ya kukagua maboresho ya mfumo huo yanayofanywa na wataalamu wa ndani kwa lengo la kuondoa changamoto zilizopo na kukidhi mahitaji halisi ya Serikali na wazabuni.