SERIKALI KUENDELEA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI ILI KUKUKUZA UCHUMI WA NCHI.
Serikali imepanga kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 133.310 kwenye sekta ya wajasiriamali wadogo na wa kati kwa kuwawezesha mitaji, kutoa mafunzo ya ujasiriamali, matumizi ya huduma za fedha, tafiti kuhusu sekta ya fedha na kuongeza matumizi ya TEHAMA kwenye sekta ya fedha.
Hayo yameelezwa jijini Mbeya na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, alipokuwa akifungua Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi” kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, yanayofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, jijini Mbeya.