SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO YA WANANCHI

Serikali imesema itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ya kufanyia biashara ili kuchochea kasi ya maendeleo kwa kukuza ajira na vipato vya wananchi kupitia uwezeshaji wa sekta mbalimbali za uzalishaji mali. Hayo yamesemwa na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), wakati akifungua Kongamano la Wahariri wa vyombo vya Habari nchini lililoandaliwa na Wizara ya Fedha, mkoani Morogoro.