SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NCHINI
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru, amewahakikishia wafanyabiashara na makampuni binafsi kwamba Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini ili kuwawezesha kuendelea kuwekeza na kukuza uchumi wa nchi.
Bw. Lawrence Mafuru ametoa ahadi hiyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC), Bw. Takashi Araki.