SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WA UMMA

Serikali imeeleza kuwa itaendelea kuboresha maslahi ya watumishi wa umma na kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili Watumishi ili kutimiza ahadi ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) alipokuwa akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo.