SERIKALI IMEPOKEA MATOKEO YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KUKABILIANA NA UVIKO-19
Serikali imepokea Matokeo ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango wa Kukabiliana na Madhara ya Kijamii na Kiuchumi ya UVIKO-19 yaani (Tanzania Covid-19 Socio-Economic Response and Recovery Plan - TCRP) kupitia fedha za mkopo nafuu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Matokeo hayo yamewasilishwa jijini Dodoma na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof. William Mwegoha, kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamadi Hassan Chande.