RC MTWARA AIPONGEZA WIZARA YA FEDHA KWA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA WANANCHI.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala, ameipongeza Wizara ya Fedha kufuatia mpango wake unaolenga kuwapa wananchi uelewa wa masuala ya Fedha ikiwemo Usimamizi wa fedha binafsi, uwekaji akiba uwekezaji, kinga za kibima na Mikopo iliyo salama kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara. Mkuu huyo wa Mkoa ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na wataalamu wa masuala ya fedha kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi shiriki, waliomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kutambulisha mafunzo hayo yatakayoendeshwa katika Wilaya zote za mkoa wa Mtwara.