RASILIMALI WATU TOKA WB CHACHU YA MAENDELEO NCHINI

Benki ya Dunia (WB) imeahidi kuendelea kuimarisha ujuzi wa Watumishi wa Benki hiyo waliopo nchini ili waweze kutoa ushauri na ujuzi utakao endelea kuchochea maendeleo ya sekta ya umma na binafsi. Hayo yamebainishwa katika Ofisi Ndogo za Hazina, jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaesimamia Rasilimali Watu, Bi. Radoslava Dimitrova Anguelova, wakati wa Mkutano kati yake na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban.