PPRA NA NEEC KUONGEZA WALIPA KODI WAKUBWA
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amesema kuwa moja ya jambo ambalo nchi inalihitaji kwa sasa ni kuwawezesha wafanyabiashara wadogo, wa kati na makundi maalumu katika ununuzi wa umma ili washiriki katika shughuli za kiuchumi na kuwa walipakodi wakubwa.
Dkt. Nchemba amesema hayo jijini Dodoma wakati wa hafla ya utiaji saini wa Hati ya Makubaliano kati ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo, wa kati na makundi maalumu katika ununuzi wa umma, ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, alikuwa mgeni rasmi.