NINDIE: WAKAGUZI WA NDANI WAIMARISHE USIMAMIZI WA VIHATARISHI.

Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Wizara ya Fedha, Mhandisi Kenneth Nindie, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa vihatarishi pamoja na kujenga uwezo wa wataalam wa ukaguzi wa ndani ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika taasisi za umma. Akizungumza wakati wa kufunga Mkutano wa 19 wa Ukaguzi kwa ngazi ya utawala, Mhandisi Nindie alisema, kuimarika kwa usimamizi wa vihatarishi kunahitaji mifumo madhubuti, uendelezaji wa ujuzi na matumizi ya fursa za mafunzo yanayopatikana, ikiwemo mafunzo yanayotolewa kwa njia ya mtandao.