NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA ZAGEUKIA MIKOPO YA NDANI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba, amesema kuwa nchi za Kusini mwa Afrika zinaangalia namna ya kuendeleza soko la ndani la mitaji kwa kutumia Hati fungani ili kuziwezesha kupata mikopo ya ndani wakati ambao mikopo mingi ya kibiashara Duniani imekuwa ikipatikana kwa gharama kubwa. Hayo yamebainishwa jijini Arusha kwa niaba yake na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Japhet Justine, wakati wa Mkutano wa Wataalamu wa masuala ya uchumi na fedha wanaosimamia madeni ya nchi zao kutoka nchi 16 za kusini mwa Afrika.