MWONGOZO WA UDHIBITI WA NDANI WA WIZARA YA FEDHA KUIMARISHA UTENDAJI

Wajumbe wa Kamati za Ukaguzi za Wizara ya Fedha wametakiwa kusimamia kikamilifu Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani wa Wizara (Internal Control Framework) ili kuboresha ufanisi wa utendaji na kufikia malengo ya Wizara yaliyokusudiwa. Hayo yameelezwa Mkoani Morogoro na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya kamati za ukaguzi za mafungu yaliyopo makao makuu ya Wizara ya Fedha kuhusu Mwongozo wa Udhibiti wa Ndani wa Wizara hiyo.