MWANDUMBYA ATETA NA UONGOZI WA SEKRETARIETI YA NCHI ZA UKANDA WA MAZIWA MAKUU

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, amezungumza na ujumbe kutoka Sekretarieti ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, ulioongozwa na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti hiyo, Mhe. Balozi João Samuel Caholo (hayupo pichani), jijini Dodoma, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Sekretarieti hiyo.