MKUU WA WILAYA YA LUDEWA AWATAKA VIONGOZI KUWA MABALOZI WA ELIMU YA FEDHA NCHINI

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Olivanus Thomas, amewahimiza viongozi wa wilaya hiyo kuwa mabalozi wa elimu ya fedha kwa wananchi ili kuwasaidia kutambua na kutumia fursa mbalimbali za kifedha zinazotolewa na Serikali na taasisi za sekta ya fedha kwa ajili ya kukuza mitaji, kuongeza kipato na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi. Mhe. Thomas ametoa wito huo wakati wa programu ya utoaji wa elimu ya fedha kwa viongozi wa Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe, iliyowakutanisha wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na taasisi mbalimbali za sekta ya fedha nchini kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu huduma za kifedha, uwekezaji na fursa za kiuchumi zinazopatikana nchini.