MKUTANO WA AFRICA 50 KUKUZA FURSA ZA UWEKJEZAJI NA MIUNDOMBINU TANZANIA.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Africa50 Bw. Alain Ebobisse, amebainisha kuwa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 (Africa50 General Shareholders' Meeting - GSM) pamoja na Jukwaa la Miundombinu Afrika (Infra for Africa Forum), ni fursa ya kuonesha mafanikio ambayo Tanzania imeyapata katika sekta ya miundombinu, kutangaza fursa zinazopatikana ikiwa ni ushahidi kuwa uwekezaji katika miundombinu ya Afrika una tija, unalipa na unaweza kufadhiliwa. Bw. Ebobisse alisema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi, Khamis Mussa Omar (MB), katika kikao cha pamoja cha maandalizi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.