MKAKATI WA MUDA WA KATI WA UKUSANYAJI MAPATO WAZINDULIWA
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amezindua Mkakati wa Muda wa Kati wa Ukusanyaji wa Mapato wa Miaka Mitatu (Medium Term Review Strategy) uliopangwa kutekelezwa kuanzia mwaka 2025/2026 hadi 2027/2028 na Kamati za usimamizi na utekelezaji wa Mkakati huo.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkakati huo, ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, Dkt. Mwamba alisema kuwa Mkakati huo unalengo la kuweka msingi imara ya ukusanyaji wa mapato, kuweka utabirifu wa sera za mapato na kuongeza makusanyo ya mapato.