MHE. MUNDE KUJIONEA UHITAJI WA KITUO CHA FORODHA NGORONGORO.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), amewasili Wilaya ya Ngorongoro, Mkoani Arusha, kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kujionea uhitaji wa kuanzishwa kwa Kituo cha Huduma za Forodha katika maeneo ya mpakani mwa Tarafa za Loliondo na Sale.
Mhe. Munde amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mhe. Luteni Kanali Robert Augustino Kakomangile, pamoja na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo.
