MHE. MUNDE ASISITIZA MATUMIZI TEKNOLOJIA KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO.
Naibu Waziri wa Fedha Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), amesisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika kuboresha ukusanyaji wa mapato, kurahisisha huduma kwa walipa kodi na kuongeza ufanisi wa mifumo ya usimamizi wa kodi.
Mhe. Munde ametoa wito huo wakati akigungua Mkutano wa 46 wa Wakuu wa Taasisi za Usimamizi wa Kodi na Wataalamu wa Kodi wa Mamlaka za Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA) unaofanyika jijini Arusha, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Munde alisema teknolojia inaendelea kubadili namna walipa kodi wanavyowasiliana na mamlaka za mapato, huku ikitoa fursa kwa Serikali kuboresha utoaji wa huduma, usimamizi wa taarifa na utii wa sheria za kodi.
