MHE. MUNDE ASHIRIKI KIKAO KUJADILI MWELEKEO WA AFRICA CREDIT RATING AGENCY (AFCRA), NEWYORK.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb.), ameshiriki katika kikao kilichojadili hali na mwelekeo wa Africa Credit Rating Agency (AfCRA), mpango wa Umoja wa Afrika (AU) unaolenga kuanzisha taasisi ya ukadiriaji wa mikopo inayomilikiwa na kuendeshwa kwa misingi ya sekta binafsi. AfCRA imeundwa kama taasisi ya kibiashara inayojigharamia na kujitegemea kifedha, tofauti na taasisi za kawaida za AU, huku African Peer Review Mechanism (APRM) ikipewa jukumu la kuongoza mchakato wa uanzishwaji wake.
Kikao kimeelezwa kuwa AfCRA inapaswa kueleweka kama taasisi ya kibiashara yenye uungwaji mkono wa kisiasa kutoka AU, huku APRM ikiwa mdhamini na kiongozi wa utekelezaji katika hatua ya uanzishwaji. Uzinduzi rasmi wa AfCRA umepangwa kufanyika tarehe 7 Oktoba 2026, jijini Port Louis, Mauritius.
