MHE. KYOBYA AWAPONGEZA WANANCHI WA IFAKARA KWA KURUDISHA MIKOPO KWA WAKATI

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Dustan Kyobya amewapongeza wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilayani Kilombero kwa kuwa na nidhamu na mikopo waliyochukua na kuirejesha kwa wakati. Mhe. Kyobya amesema hayo wakati akifungua program maalum ya Elimu ya Fedha kwa Umma inayoendeshwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na washirika mbalimbali wa sekta ya fedha nchini iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo – Ifakara, Mkoani Morogoro.