MHE. DKT. NCHEMBA ATETA NA BALOZI WA HUNGARY
Balozi wa Hungary hapa nchini mwenye Makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya, Mhe. Zsolt Mészáros, ameipongeza Tanzania kwa kusimamia vema sera zake za fedha na uchumi, hatua iliyoifanya iendelee kuimarika kiuchumi na kuahidi kuwa nchi yake itaongeza ushirikiano kwa faida ya nchi hizo mbili.
Mhe. Mészáros ameyasema hayo, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.