MHE. DKT. NCHEMBA AISHUKURU BENKI YA UBA KWA USHIRIKIANO WAO KATIKA MIRADI YA MAENDELEO
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameishukuru United Bank of Africa (UBA), kwa kuwa tayari kushirikiana na Serikali katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.
Dkt. Nchemba, ametoa shukrani hizo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank of Africa (UBA), Bw. Gbenga Makinde, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam.