MHE. CHANDE AWATAKA WATANZANIA KUWA WAZALENDO KATIKA KUTOA NA KUDAI RISITI ZA EFD

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), amewataka watanzania kuwa wazalendo zaidi katika kutoa na kudai risiti ya mashine za Kieletroniki (EFD), ili kuhakikisha mapato ya nchi yanaongezeka na kusaidia kutekeleza miradi na huduma mbalimbali za kijamii. Mhe. Chande, alitoa rai hiyo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Kata ya Kiusa, Wilaya ya Moshi Mjini, Mkoani Kilimanjaro, akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo iliyolenga kutatua changamoto mbalimbali wanazopitia wafanyabiashara mkoani humo na kuhamasisha matumizi sahihi ya mashine za Kieletroniki (EFD).