MHE. CHANDE AWAAGIZA CHUO CHA KODI KUFANYA TAFITI ZA MFUMO WA UKUSANYAJI WA KODI

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), amekiagiza Chuo cha Kodi kufanya tafiti mbalimbali ambazo zitatoa suluhu ya changamoto zinazoukabili mfumo wa ukusanyaji kodi. Ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam katika Mahafali ya Kumi na Sita ya Chuo cha Kodi yaliyofanyika katika ukumbi wa Multipurpose. Alisema tafiti hizo pia ziibue vyanzo vipya vya mapato, namna bora ya kudhibiti ukwepaji kodi pamoja na kufanya ulipaji kodi uwe rahisi na rafiki kwa kuzingatia teknolojia za kisasa zilizopo duniani.