MHE. CHANDE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA MWAKA WA KUDHIBITI FEDHA HARAMU NCHINI BOTSWANA

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu (Eastern and Southern Africa Anti Money Laundering Group (ESAAMLG), unaofanyika katika mji wa Kasare, nchini Botswana, kuanzia tarehe 8 -9 Septemba, 2023. Mkutano huo wa siku mbili, pamoja na mambo mengine, utajikita katika kujadili mifumo na mbinu mbalimbali za udhibiti wa fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa silaha za maangamizi katika nchi wanachama wa ESAAMLG.