MHE. CHANDE AKAGUA MIRADI MIPYA CHUO CHA UHASIBU (IAA)

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameupongeza uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kwa matumizi na usimamizi nzuri wa fedha za miradi ya ujenzi wa miundombinu ya Chuo hicho ambayo amesema imejengwa kwa viwango vinavyolingana na thamani ya fedha iliyotumika. Mhe. Chande alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa miradi inayoendelea katika Chuo hicho ukiwemo ujenzi wa jengo la Postgraduate na Hosteli, inayotekelezwa kupitia mfumo wa "force account".