MHE. CHANDE AITAKA TIRA KUDHIBITI KAMPUNI ZA BIMA ZINAZOFANYA UBABAISHAJI

Serikali imeiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) kuzichukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuzifutia leseni za kufanyabiashara nchini kampuni za Bima zinazoshindwa kutekeleza wajibu wao wa kuwalipa wateja wao fidia za majanga mbalimbali kwa wakati na kwa kuzingatia thamani halisi ya mali zilizokatiwa bima husika. Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande, alipotembelea na kukagua mabanda ya waoneshaji katika maadhimisho ya pili ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Rock City Mall, jijini Mwanza.