MHE. BALOZI OMAR AZINDUA OFISI ZA TRA ZINAZOTEMBEA

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), leo tarehe 25 Februari 2026, amezindua Ofisi zinazotembea (Magari Maalum) mawili katika maeneo ya kibiashara ya Mwenge na Tegeta, Jijini Dar es Salaam, yatakayotumiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhudumia wateja (Walipakodi) katika maeneo mbalimbali nchini. Magari hayo maalumu ni sehemu ya magari kumi ya aina hiyo ambayo Serikali Kupitia Wizara ya Fedha, imeipatia TRA wa ajili ya kuwahudumia wananchi hususan katika maeneo ambayo Walipakodi watakuwa na changamoto ya kutumia mifumo ya TEHAMA ya TRA ya masuala ya kodi kutokana na ukosefu wa mtandao wa Intaneti.