MHE. BALOZI OMAR ATAKA KASI ZAIDI UJENZI WA SGR KIPANDE CHA TATU

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, amewataka wakandarasi wanao jenga Reli ya Kisasa (SGR) kuongeza kasi ili kufidia muda uliopotea kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza, na kuzingatia ubora wa kazi na masuala ya mazingira na jamii. Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa(SGR), katika vipande vya tatu, nne na tano, Mhe. Balozi Omar alisema Serikali inataka kuona mradi huo unatekelezwa kwa kasi zaidi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuunganisha maeneo mbalimbali ya nchi kwa njia ya reli ya kisasa.