MHE. BALOZI OMAR AHITIMISHA ZIARA YAKE TRA

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amehitimisha ziara yake ya siku mbili katika Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA jijini Dar es Salaam. Leo, tarehe 27 Februari, 2026, alitembelea Idara ya Forodha, Kitengo cha Ufuatiliaji wa Usafirishaji (Transit Monitoring), Idara ya Upelelezi wa Kodi, Idara ya Kodi za Ndani na Timu ya inayosimamia Mfumo Mpya Jumuishi wa Kodi za Ndani (IDRAS). Mhe. Balozi Omar ameielekeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuimarisha usimamizi wa mizigo inayoingia nchini kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nchi jirani (transit), ili kudhibiti vitendo vya ukwepaji kodi vinavyofanywa na baadhi ya wadau wa forodha wasio waaminifu.