MHE BALOZI OMAR AFIKA KUJITAMBULISHA CCM DODOMA
Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa, alipotembelea Ofisi za Chama hicho, ngazi ya Mkoa, kujitambulisha.
“Nimekuja kwenye Ofisi za Chama kujitambulisha baada kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Waziri wa Fedha, ni mkazi sasa wa Dodoma, mwanachama hai wa CCM, nikaona ni vema nije kujitambulisha” Alisema Mhe. Balozi Omar
