MFUKO WA MAENDELEO WA ABU DHABI KUENDELEA KUFADHILI MIRADI YA MAENDELEO TANZANIA

Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi wa Umoja wa Falme za Kiarabu umeahidi kutoa mkopo nafuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania ukiwemo mradi wa umeme wa Benaco-Kyaka, mkoani Kagera na ujenzi wa makazi ya watumishi ya gharama nafuu Visiwani Zanzibar, inayokadiriwa kugharimu dola za Marekani milioni 420.