MCHANGO WA KAMPUNI ZENYE UMILIKI MDOGO WA SERIKALI WAONGEZEKA
Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) amesema kuwa mchango wa Kampuni ambazo Serikali ina umiliki wa Hisa Chache katika Mfuko Mkuu wa Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina umeongezeka kutoka shilingi bilioni 58.26 mwaka 2020 hadi shilingi bilioni 266.52 mwaka 2024.
Hayo yamebainishwa katika Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Wakurugenzi wa Bodi za Kampuni ambazo Serikali ina umiliki wa Hisa Chache, uliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU), jijini Arusha.
