MAWAZIRI WATATU WAJADILI MAENDELEO YA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde (Mb), wamekutana na kufanya mazungumzo jijini Dodoma kuhusu maendeleo ya Sekta ya madini na uwekezaji ili kuendelea kukuza Uchumi wa nchi. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza Johari, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine na wajumbe wengine kutoka Wizara hizo tatu.