MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YAHIMIZWA MKUTANO WA 10 WA WAKAGUZI AFRIKA

Wakaguzi wa Ndani barani Afrika wametakiwa kubadilishana uzoefu na kutumia teknolojia katika kutatua changamoto mbalimbali katika taaluma yao na kuhakikisha wanasaidia taasisi na Serikali zao kuboresha ufanyaji kazi ili kuchochea maendeleo. Hayo yameelezwa jijini Arusha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, wakati wa Mkutano wa 10 wa Wakaguzi wa Ndani Barani Afrika, ulioanza kwa mikutano midogo inayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).