MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA NAIROBI-KENYA
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba, pamoja Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El Maamry Mwamba wakiwa katika matukio mbalimbali kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21), unaofanyika tarehe 29 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya.