MAREKANI YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KWA KASI ZAIDI

MAREKANI imeahidi kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika jitihada zake za kuimarisha uchumi wake na maendeleo ya wananchi kwa kutoa fedha na ujuzi mbalimbali pamoja na kuvutia uwekezaji kupitia ubia kati ya sekta ya Umma na Binafsi. Ahadi hiyo imetolewa na Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Michael Battle, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, katika Ofisi Ndogo za Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam, alipofika kujitambulisha.