MAKONGAMANO YASAIDIA MABORESHO 57 YA KODI MWAKA 2023/24

Makongamano ya Kodi yanayofanywa na Wizara ya Fedha kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wananchi wa kawaida yamewezesha kufanyiwa maboresho kwa zaidi ya maeneo 57 ya kikodi katika mwaka wa Fedha 2023/2024 huku hatua hiyo ikilenga kusisimua ufanyaji biashara, kulinda viwanda vya ndani na kuchochea uwekezaji nchini. Hayo yamesemwa Jijini Mwanza na Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, wakati timu ya watalaam wa masuala ya fedha na uchumi wa Wizara ya Fedha ilipokusanya maoni ya kuboresha kodi kwa ajili ya Mwaka wa Fedha 2024/2025.