MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA AWASILI NCHINI KUTETA NA MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Kusini Mashariki mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa, amesema kuwa lengo la ziara yake nchini Tanzania ni kujitambulisha na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Benki hiyo baada ya kuchukua nafasi ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Benki hiyo Kanda ya Kusini Mashariki mwa Afrika Dkt. Hafez Ghanem, ambaye amestaafu.
Akiwa nchini, Bi. Kwakwa, anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam, baadae ataelekea Visiwani Zanzibar ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na atakutana pia na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na viongozi wengine kadhaa wa Serikali.