MAADHIMISHO YA WIKI YA FEDHA YAFANA JIJINI MBEYA

Mchumi kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Felista Malibate (Kulia), akitoa elimu ya fedha kwa Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Uyole-Mbeya (CDTI), walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.