MAADHIMISHO WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KUWASOGEZEA WANANCHI HUDUMA ZA FEDHA KARIBU

Serikali inafanya maadhimisho ya pili ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ili wananchi waweze kupata elimu ya fedha na kuweza kufahamu fursa, bidhaa na huduma mbalimbali zilizopo kwa lengo la kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa nchi. Hayo yameelezwa jijini Mwanza na Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamwaja alipokutana na wanahabari wakati akizungumza kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa inayofanyika mkoani humo kuanzia Novemba 21 hadi 26, 2022.