MAADHIMISHO WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KUINUA UCHUMI JUMUISHI

Serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wengi wanapata uelewa wa masuala ya fedha ili kuwawezesha kushiriki katika uchumi jumuishi na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi. Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Kamishna wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Charles Mwamwaja alipokutana na wanahabari kuzungumzia Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa inatarajiwa kufanyika mkoani Mwanza kuanzia Novemba 21 hadi 26, 2022 yenye kauli mbiu “Elimu ya Fedha kwa Maendeleo ya Watu”.