KOREA YAIPATIA TANZANIA SH. TRILIONI 2

Serikali ya Tanzania na Jamhuri ya Korea zimetiliana saini mikopo nafuu ya jumla ya dola za Marekani bilioni moja sawa na shilingi trilioni 2.3 kutoka Mfuko wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Korea (EDCF) kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.