KISHINDO BAJETI WIZARA YA FEDHA 2025/26 IKIPITA

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha kwa kishindo bajeti ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2025-2026 ya kiasi cha Sh. trilioni 20.19 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mafungu yake nane (8) ya kibajeti. Awali Mhe. Dkt. Nchemba alitoa maombi ya kuidhinishiwa kiasi hicho wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Fedha bungeni Jijini Dodoma, ili iweze kutekeleza vipaumbele vyake vitano ilivyopanga kuvitekeleza katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.