KILIMANIHEWA KUPEWA ELIMU NAMNA YA UTUNZAJI NA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA

Wafanyabiashara wametakiwa kujenga tabia ya kuweka akiba katika biashara zao ili kuhakikisha wanakuwa na maendeleo endelevu. Afisa Sheria Mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonza, alitoa wito huo alipokuwa akitoa elimu ya utunzaji na matumizi sahihi ya fedha katika ziara ya utoaji elimu ya fedha kwa umma wilayani Masasi mkoani Mtwara.