KILELE CHA MAONESHO YA NANE NANE
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta ya Binafsi (PPP Centre), Bw. David Kafulila (wa pili kushoto), kuhusu majukumu ya Kituo hicho, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.