KATIBU TAWALA MKOA WA SONGWE ATEMBELEA MAADHIMISHO WIKI YA FEDHA KITAIFA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda (Kushoto), akimsikiliza Afisa Usimamizi Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Jackson Mushumba, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kaulimbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi”, yanayofanyika katika Viwanja vya Ruanda-Nzovwe, Jijini Mbeya, ambayo yamezikutanisha Taasisi Ndogo za Fedha, Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na wajasiriamali kutoka mkoa wa Mbeya na mikoa jirani.