KATIBU TAWALA MKOA WA MOROGORO ASISITIZA MATUMIZI BORA YA FEDHA KWA WAJASIRIAMALI
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ally Mussa, amewataka wajasiriamali wa Mkoa huo kuwa na matumizi bora ya fedha wanazozipata katika shughuli zao mbalimbali za uzalishaji mali ili kuepukana na mikopo isiyo rasmi (mikopo umiza).
Dkt. Mussa alisema hayo wakati wa kikao na timu ya kutoa elimu ya fedha kwa Umma kutoka Wizara ya Fedha ambayo ipo Mkoani Morogoro kutoa elimu hiyo kwa makundi mbalimbali ya wananchi katika halmashauri saba (7) za Mkoani wa Morogoro.