KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE- PAC YARIDHISHWA NA UJENZI JENGO LA WIZARA YA FEDHA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Devotha Minja, ameipongeza Wizara ya Fedha kwa kutekeleza Mradi wa Jengo jipya la Ofisi ya Wizara lililopo Mji wa Serikali Mtumba, kwa ufanisi, kwa kuwa mradi huo hauna maswali mengi ikilinganishwa na miradi mingine waliyoitembelea. “Kazi ni nzuri, mmefanya kazi kubwa na taarifa zinazohitajika ziwasilishwe ili tuweza kuishauri vema Serikali”, alisema Mhe. Minja. Aidha Mhe. Minja kwa niaba ya Kamati ameahidi kutoa ushirikiano katika maeneo mbalimbali yanayoihusu Wizara ya Fedha kwa Maendeleo ya Wananchi.