IMF NA BENKI YA DUNIA ZAITEUA TANZANIA KUNUFAIKA NA MPANGO WA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (World Bank Group), zimeitangaza Tanzania kuwa nchi ya pili, baada ya Madagascar, kunufaika na Mfumo wa Ushirikiano wa Kuimarisha Hali ya Hewa kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na athari mbaya za uharibifu wa mazingira.
Kupitia Mfumo huo, IMF na WBG watafanya kazi kwa karibu na washirika wengine wa maendeleo, kuratibu juhudi zao za kuunga mkono ajenda ya mageuzi ya sera ya Tanzania ili kukabiliana na vihatarishi na changamoto zinazohusiana na mabadiliko hayo ya tabianchi na kuimarisha ustahimilivu wa uchumi wa Tanzania.